
Neno & Maombi
Kujenga maisha ya kiroho kwa kujifunza Neno la Mungu na kudumu katika maombi.
Idara ya Vijana · CA's
Mahali pa vijana kukua katika Kristo, kujenga vipawa, kushuhudia Injili na kutumika kwa uaminifu.

Kukua · Kutumika · Kuongoza
CA's inalenga kuwajenga vijana kiroho na kuwaandaa kutumia vipawa vyao katika kanisa na jamii. Maisha ya idara yanajengwa katika Neno la Mungu, maombi, ushirika, ushuhudiaji na huduma.
Maisha ya CA's

Kujenga maisha ya kiroho kwa kujifunza Neno la Mungu na kudumu katika maombi.

Kuwafikia wengine kwa Injili ya Yesu Kristo na kuishi kama mashahidi wake kila siku.

Kutambua, kukuza na kutumia vipawa katika huduma mbalimbali za kanisa.

Kujenga mahusiano yenye afya, kuwajibika na kukuza kizazi cha watumishi na viongozi.
Tunachofanya
Semina na mafundisho, maombi, ushuhudiaji, michezo, outing na huduma za kijamii hutengeneza nafasi za vijana kukua, kushirikiana na kutumika.
Matukio katika Picha ↓
Kuna nafasi yako
Jiunge na familia ya CA's na uwe sehemu ya vijana wanaomfuata Kristo, wanaojifunza na wanaotumia vipawa vyao kwa utukufu wa Mungu.